Thursday, September 7, 2017

Spika Ndugai: STAMICO imewaangusha Watanzania

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Shirika la Madini la Taifa (Stamico) ni muhimu, hivyo Wizara ya Nishati na Madini inapaswa kulitazama upya kuona namna ya kuliboresha ili liwe jipya kwa kuwa limewaangusha Watanzania.

Ndugai amesema hayo leo Septemba 7 Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati wa kukabidhi kwa Rais John Magufuli ripoti za kamati alizoziunda kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya tanzanite na almasi.

Spika amesema wawekezaji wengi wanaokuja nchini ni wazuri lakini wakikuta mifumo ya kuwasimamia ipo ovyo nao huanza mambo ya ovyo.

“Kamati zote zinazungumzia mikataba ambayo ni ya kawaida sana. Kikubwa Watanzania tuwe wazalendo na kushikamana. Wakati wa Mwalimu Julius Nyerere alijaribu kupingania rasilimali zetu ikafika hatua dawa ya meno ikakosekana madukani lakini Watanzania waliendelea kumuunga mkono,” amesema Ndugai.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )