Thursday, September 14, 2017

Umoja wa Mataifa Waituhumu Tanzania kwa Kushirikiana na Korea Kaskazini Kuboresha Mfumo wa Makombora ya Kivita

Umoja wa Mataifa unaichunguza Tanzania kwa tuhuma za kikuikwa vikwazo vya kisilaha ilivyoiwekea Korea Kaskazini ambapo inadaiwa kuwa licha ya vikwazo vilivyowekwa, Tanzania imeendeleza biashara ya silaha na nchi hiyo..

Ripoti ya Septemba 9 ilitolewa siku mbili kabla ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa pamoja kuweka vikwazo vipya vinavyo ishinikiza Korea Kaskazini kufanya mazungumzo juu ya silaha zake za nyuklia.

Jopo la watu wanane limesema linafanya tathmini juu ya taarifa kutoka kwa vyanzo vya habari vya nchi wanachama wa UN ambavyo havijatajwa majina vikisema kuwa Tanzania iliingia mikataba ya kijeshi na Korea Kaskazini yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 12.5.

Kampuni ya Haegeumgang Trading Corporation  ya Korea Kaskazini inasemekana kuwa inafanya ukarabati na kurekebisha mifumo ya makombora ya kivita nchini Tanzania  na ulinzi wa anga ( Rada) kuifanya iwe ya kisasa.

“Serikali ya Tanzania mpaka sasa bado haijatoa maelezo kujibu mambo ambayo yamedadisiwa na jopo hilo,” wachunguzi wa UN wamesema.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje, Dr. Suzan Kolimba amesema kuwa hawajapokea taarifa yoyote kutoka UN na hivyo kwa sasa hawawezi kuzungumza kuhusu madai hayo yaliyotolewa.

Mbali na Tanzania, mataifa mengine yanayochunguzwa na UN ni kwa kuendeleza biashara na Korea Kaskazini ni Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Eritrea, Msumbiji, Namibia, Syria na Uganda.

Korea Kaskazini imekuwa ikiwekewa vikwazo mbalimbali siku za karibuni kutokana na kuendelea na majaribio ya silaha za nyuklia kinyume na makubaliano ya UN.

Kiongozi wa nchi huyo, amewahi kunukuliwa akisema kuwa nchi hiyo kwa sasa ina makombora makubwa yanayoweza kulenga sehemu yoyote ya dunia

==> Unaweza kuisoma ripoti ya UN hapa chini;
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )