Friday, September 29, 2017

Wanaume Wa Mauritania Huwalazimisha Binti Na Wake Zao Kutumia Mitishamba,vyakula Na Vinywaji Hivi Ili Wanenepe .......Sababu Itakushangaza.

Mauritania  ni  nchi  inayo patikana  upande  wa  kaskazini  magharibi  mwa  bara  letu  tukufu  la  Afrika.Katika  nchi  hii  wanaume  huwanenepesha wake  pamoja na  binti  zao.


Zoezi  hili  la  kuwanenepesha  wake  pamoja  na mabinti  hufanywa kwa  kutumia  dawa  za  mitishamba, vyakula  na  vinywaji  mbalimbali.

Kwa  upade  wa  mabinti, zoezi  hili  hufanyika  binti  anapokuwa  ametimiza  miaka  saba hadi  kumi na  mara  nyingi hufanyika wakati  wa likizo.

Mabinti  hawa  huwekwa  katika  camp  maalumu    ambako  hutakiwa  kula  vyakula, vinywaji  na  mitishamba  ya  aina  mbalimbali  iliwaweze  kunenepa.

VYAKULA  WANAVYO  LISHWA
Mabinti  hawa  hulishwa  vyakula  vya  aina  mbalimbali. Baadhi  ya  vyakula  hivyo  ni  kama  ifuatavyo :

1.     Vyakula  vyote  vitamu  vitamu  na  vyenye  sukari nyingi
2.     Vyakula  vyenye  mafuta  mengi
3.     Uji  wa  ulezi 
4.     Uji  wa  ufuta
5.     Asali  ya  tende  ( Date  Syrup )
6.     Maziwa  ya  mbuzi
7.     Maziwa  ya  ngamia
8.     Mitishamba  ya  aina mbalimbali  ambayo  husaidia  kunenepesha mwili
9. Vyakula  vyenye ngano  kwa  wingi, pamoja  na  vyakula  vya  wanga  kwa  wingi.

9.     Pamoja  na  vyakula vingine vya  aina  tofauti tofauti  ambavyo  vinahusika  na kumfanya mtu  anenepe.

Zoezi  hili  hufanyika  kwa  umakini  mkubwa bila  kuleta  utani  wa  aina  yoyote  ile.  Matrons  wanao simamia  zoezi  hili, huwa wanakuwa  serious  sana  ili kuhakikisha  kila  mtoto  wa kike  alie kwenye  camp  anakula  na  kutumia  kiasi  cha  chakula  na  mitishamba anayo  takiwa  kuitumia  kwa  kipindi kilicho elekezwa.
 
Na  ikitokea  binti akaleta  ubishi, basi  atalishwa  kwa  lazima  na  ikitokea  binti  huyo  akajitapisha  chakula, kinywaji  au  kimiminika  cha  mitishamba  alicho pewa  kutumia, basi  matrons  watamtisha  kwamba, endapo  atatapika, atalazimishwa  kula  matapishi  yake.
 
Zoezi  hili huendelea  pindi  binti  anaporudi nyumbani  kwa wazazi  wake  na hufanyika  kila siku hadi  utakapo  fika  wakati  wake  wa  kuolewa.
 
Akiwa  kwa  wazazi  wake, binti  atatakiwa  kuwa  anatumia  kila siku vimiminika  vinavyo tokana  na   mitishamba  inayo saidia   kunenepesha mwili  pamoja  na vinywaji  & vyakula, vinavyo saidia  kunenepesha  mwili.

Zoezi hili  hufanyika  kwa  umakini  mkubwa sana. Wazazi  wa  wabinti huwa  makini  na  wakali  katika  kuhakikisha  binti  yao  anazingatia  kutumia  vyakula  hivyo  pamoja  na  mitishamba  hiyo  ya  kunenepesha  mwili.

BAADA  YA  KUOLEWA
Hata  baada  ya  kuolewa, mwanamke  huyo  hutakiwa  kuendelea  kutumia  vyakula na mitishamba  ya kunenepesha  on daily  basis.  Mume  huwa  makini  sana  na  humsisitizia  mkewe  kutumia  mitishamba  na vyakula  vya  kunenepesha.

NI  UTAMADUNI  WAO  TOKA  KALE
Kuwalazimisha mabinti  pamoja  na  wake kutumia vyakula  na  mitishamba  ya  kunenepesha  mwili, ni  utamaduni  wa  watu wa  Mauritania  tangu  enzi  na  enzi.

Zoezi  hili  hufanyika  kama  sehemu  ya  kuenzi  utamaduni  huo  ulio  jikita  mizizi  miongoni  mwa  wananchi  wa  Mauritania.

SABABU  GANI  HUWAFANYA  WANAUME  WA  MAURITANIA  KUWANENEPESHA  BINTI  ZAO  NA  WAKE  ZAO.
Sababu  kuu  inayo  wafanya  wanaume  wa  Mauritania  kuwanenepesha  wake  na  binti zao  ni  dhana  iliyo jengeka
i.          Dhana  iliyo jengeka  miongoni  mwa  jamii  ya  wana Mauriutania  kwamba, mwanamke  mnene  ndio  mrembo. Kwa  wana Mauritania, ili  mwanamke  aweze  kuonekana  mrembo  ni  lazima  awe  mnene.
 
Kama  sio mnene  basi  hawezi kuchukuliwa  kama  mrembo  na  ni vigumu  sana  kuolewa.
Pindi  kijana  anapo peleka  taarifa  kwa  wazazi  wake  kwamba  amepata  mchumba  na  kwamba  anataka  kumuoa,  swali  la  kwanza  analo  ulizwa  ni  kama  mwanamke  huyo  ni  mnene  au  la, na  kama  mwanamke  huyo  si mnene, basi  familia  nzima  wataipinga  na kuisusia  ndoa  hiyo.    

Hivyo  basi  katika  kuhakikisha  mabinti  zao  wana  fit in kwenye jamii, wana  Mauritania  huhakikisha  kuwa  binti  zao  wanakuwa  wanene  kwa kufanya  zoezi  hilo  la kuwanenepesha  tangu  wakiwa  wadogo.

ii.        Sababu  ya  pili  ni  FAHARI  kwa  wazazi  na mume.  Baba  na  mama  mzazi  ni  fahari kwao  kumuoza  binti  yao  akiwa  mnene  vilevile  mume  ni fahari kwake  kuwa  na mwanamke  mnene na pia kuendelea  kudumisha  unene  wake hata  baada  ya  kufunga  ndoa.
Kwa  wana  Mauritania  wengi, unene  ni  ishara  ya  kuwa  na  maisha mazuri  yenye  neema. Ishara  ya  kutokuwa  na  njaa. Hivyo  basi kuruhusu  binti au  mke  wako  kukonda, itakufanya  uonekane  wewe  hauna  maisha mazuri.

Hauna  uwezo  wa  kuwatunza  binti  zako na mke  wako.

Mashirika  mbalimbali  ya  kutetea haki za  binadamu  na  haki  za  wanawake  yamekuwa  yakijitokeza  hadharani  kupingana  na  desturi  hii, lakini  bila  mafanikio  kwani  imethibitika  kuwa  wana  Mauritania  wengi  bado  wana  amini  katika desturi  hii na  kwamba  ni  vigumu  sana  kuiacha  kwa  mara  moaja.
 
KUNENEPA  NI RAHISI  SANA  KULIKO KUPUNGUA
Kunenepa  ni  rahisi  kuliko  kupungua. Duniani  hakunaga  mtu  mwembamba. Uzoefu  unaonyesha  kuwa, mtu  anae taka  kunenepa anaweza  kupata  matokeo ya haraka  zaidi  kuliko  Yule  anae  taka  kupungua.

Hii  ni  kwa  sababu  njia  za  kunenepa  ni rafiki zaidi kwa  mtu  anaetaka  kunenepa  kuliko  ilivyo kwa  njia  za  kupungua  mwili.

Kwa mfano, mtu  anaetaka  kupungua  pamoja  na  mambo  mengi  kama  kutumia  dawa, anaweza  kutakiwa  pia  kufanya  mazoezi  ya  mara  kwa  mara, kufanya  diet  na  kuachana  na  baadhi  ya  vyakula, jambo  ambalo  ni  tofauti  na  mtu  anaetaka kuongeza na kunenepesha  mwili.

LISHE   YA  KUNENEPESHA  MWILI
Kama mwili  wako  ni  mwembamba  au  umedhoofika  kutokana  na  maradhi  ya  sababu  mbalimbali  kama  vile  stress  nakadhalika, ipo DAWA  LISHE  YA  KUNENEPESHA  MWILI.  Dawa  hii ni  ya  asili  na  itasaidia  kunenepesha  mwili  wako  na  kuurudisha  katika  hali  yake  ya  kawaida.

Kwa  mahitaji  ya  Dawa  Lishe  ya  kunenepesha  mwili, fika  katika  duka  la  Neema  Herbalist  lililopo  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM, jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING   nyuma  ya  jingo  la  UBUNGO  PLAZA.

Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba 0766 53 83 84.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )