Thursday, September 7, 2017

Waziri Mkuu Atoa Maagizo Mazito Wizara ya Kilimo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na Bodi ya Korosho Tanzania zifanye tathimini ya maandalizi ya msimu ujao kwa wakati na zimpatie taarifa mara moja ili kama yapo matatizo yatatuliwe kwa muda.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo  wakati akizungumza na wadau wa zao la korosho kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake mjini Dodoma kujadili mwenendo wa zao la korosho na ununuzi wa pembejeo.

"Lipo tatizo la tathmini ya maandalizi ya msimu kutofanyika kwa wakati na kusababisha matatizo kutotatuliwa kwa wakati. Bodi na Wizara zitoe tathimini ya maandalizi ya msimu ujao kuhusu vyama vya ushirika vilivyojipanga, upatikanaji wa vifaa kama magunia na nyuzi, maghala, masoko, mizani, minada, malipo na mfumo wake," alisema.

Aidha Mh Majaliwa amesema tangu serikali iamue kusimamia mazao makuu matano ya pamba, chai, kahawa, korosho na tumbaku hajapata muda wa kukaa na kuongea na wadau wote.

 "Serikali imeamua kufuatilia usimamizi wa mashamba; kusimamia upatikanaji wa mbegu, miche na pembejeo; kufuatilia uvunaji na mfumo wa masoko ya korosho na pia kufuatilia mfumo wa ushirika katika baadhi ya mazao. Kwa sasa zao la korosho linalimwa katika wilaya 50 kwenye mikoa 11 ya Dodoma, Iringa, Lindi, Mbeya, Morogoro na Mtwara. Mingine ni Njombe, Pwani, Ruvuma, Singida na Tanga. Ameongeza

Ameongeza kwamba "Katika msimu wa mwaka 2016/2017 zao la korosho lilikuwa ni moja kati ya mazao ya kibiashara yenye tija na faida nyingi kwa kuliingizia Taifa fedha za kigeni kiasi cha dola za Marekani milioni 346.6," alisema na kuongeza kuwa katika msimu wa mwaka 2017/2018 watendaji hawana budi kujipanga vizuri ili zao la hilo liendelee kuliingizia Taifa dola nyingi zaidi kwa kuwa Serikali imetoa viatilifu bure. 

 "Ninasisitiza eneo hili kwa sababu tumebaini kuwa korosho inachangia zaidi ya asilimia 50 ya mapato kwenye Halmashauri zinazolima kwa wingi zao hilo. Kwa kuwa zao hili ni la kimkakati, naitaka Wizara inipatie taarifa sahihi na kwa wakati," alisisitiza.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )