Wednesday, September 6, 2017

Wizara ya Ardhi yaanza kutoa hati ya miaka 99 kwa wakazi wa Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  imeanza kutoa hati mpya za ardhi zenye umri wa miaka 99 tofauti na zile zilizokuwa zikitolewa awali za miaka 33.

Akizungumza na wanahabari jana  Mjini Dodoma Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema  zoezi hilo la ubadilishaji wa hati kwa wakazi elfu 25 wa mkoa huo limeanza rasmi ambapo wakazi hao wanatakiwa kufika Wizarani wakiwa na nakala za hati zao za zamani ambazo zimelipiwa kodi zote za ardhi.

“Ubadilishaji wa hati hizi ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipoivunja Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ambapo aliiagiza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kubadilisha hati zilizokuwa zikitolewa na mamlaka hiyo kutoka umiliki wa miaka 33 na kuwa miaka 99,” alifafanua Lukuvi.

Aliongeza kuwa hati hizo za miaka 33 zilikuwa zikiwanyima fursa wakazi wa Dodoma kupata wawekezaji kutoka nje ya nchi kutokana na hati hizo  kuwa za muda mfupi tofauti na hati zinazotolewa na miji mingine hapa nchini.

Aidha hati hizo pia zilikuwa kikwazo kwa wamiliki kushindwa kupata mikopo mikubwa ambayo hutolewa kwa watu wenye umiliki wa ardhi wa kuanzia miaka 50 na kuendelea.

Lukuvi amesema kuwa mabadiliko hayo ya hati hayata athiri mipaka ya viwanja vitakavyobadilishiwa hati bali kinachofanyika ni kubadilisha umri wa umiliki wa ardhi.

==>Msikilize hapo chini
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )