Tuesday, October 10, 2017

Diwan Amchana Mbowe......Amtaka Amrudishe Dr Slaa

Mmoja wa Madiwani ambao wamehamia CCM wakitoka CHADEMA mkoani Arusha waliokumbwa na skendo ya kununuliwa, amemtaka Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, kumtafuta aliyekuwa katibu wake Mkuu Wilbroad Slaa, ili kuokoa jahazi kwenye chama.

Kwenye video iliyoambaa ambayo anaonekana akizungumza,  aliyekuwa diwani wa kata ya Kimandolu Mchungaji Rayson Ngowi, amesema kuna haja ya kutafuta hekima za Wilbroad Slaa, ili kukisaidia chama hicho kukaa kwenye mstari unaofaa, kwa kuwa sasa kimeanguka kwa kiasi kikubwa.

Bwana Ngowi amesema hata yeye kutoka CHADEMA ameondoka kwa kutaka mwenyewe na sio kununuliwa kama inavyodaiwa, na kwamba kuna wengine watakaofuata nyuma yao baada ya wao kuondoka kwenye chama hicho.

“CHADEMA ya leo sio ile ya Dkt Slaa, CHADEMA ya leo ni  ya maslahi, CHADEMA ganganjaa, na wakikataa mimi nitasema, sikiliza Mbowe, chama chako kina matatizo makubwa, huna viongozi, kamtafute Dkt. Slaa nafikiri ataokoa jahazi, kama mnataka kurudisha imani, kwa sababu sio mimi tu nimeondoka watakuja wengi”, amesema diwani huyo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )