Friday, October 6, 2017

Ester Bulaya: Ninafuatiliwa na watu waliovaa mavazi ya kininja

Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA), Ester Amos Bulaya, amesema kuwa yupo katika hatari kubwa kutokana na kufuatiliwa na watu waliovalia mavazi ya kininja nyumbani kwake wilayani Bunda.

Bulaya ametoa taarifa hiyo alipokuwa leo  na kusema kwamba watu hao walimfuata nyumbani kwake wakiwa na gari aina ya Noah huku wamevaa kininja.

Aidha, amesema kuwa kwa bahati nzuri wakati watu hao wakienda kwake hakuwepo nyumbani, hivyo ndugu zake wakampigia simu ili asirudi nyumbani siku hiyo aweze kuokoa usalama wake..

Hata hivyo, ameongeza kuwa watu hao waliokuwa wakimtafuta walizunguka kwa baadhi ya ndugu zake akiwemo bibi yake na kumkosa, lakini alienda kutoa taarifa polisi na mkuu wa kituo kuanza kufuatilia suala hilo, lakini haikuchukua muda akahamishwa kituo cha kazi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )