Wednesday, October 4, 2017

Kauli ya Paul Makonda Baada ya Rais Magufuli Kudai ni Mfano wa Kuigwa

Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kutaka Wakuu wa mikoa wengine kuiga utendaji kazi wa Paul Makonda ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,  Mkuu wa mkoa huyo amemshukuru Rais Magufuli na wananchi wa Dar es salaam kwa kumpa ushirikiano.

RC Makonda ametoa shukrani hizo  kupitia ukurasa wake wa instagram huku akitaka pongezi za Rais Magufuli ziwaendee wale wote waliomuunga mkono.

"Utukufu na heshima apewe Mungu aketie mahali patakatifu.Asante sana Mh Rais asante watumishi wa Mkoa wa Dar es salaam. 

"Asante sana wadau na Wananchi wote wa mkoa wa Dar es saalam kwa mshikamano wenu,Upendo wenu na Umoja wenu katika kuleta maendeleo ya mkoa wa Dar es salaam.

"Pongezi za Mh Rais ziende kwenu nyote mnaoendelea kuunga mkono Kwa hali na mali maendeleo ya Mkoa wa Dar es salaam."
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )