Monday, October 30, 2017

Kigwangalla Anasa Jangili Likiwa na Risasi 356

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Masalu Wella Nangale wa kijiji cha Mwasengela Meatu Simiyu amekamatwa akijipanga kuelekea Moru ndani ya hifadhi ya Serengeti akiwa na malengo ya kwenda kufanya mauaji kwa wanyama aina ya Faru.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amethibitisha kukamatwa kijana huyo na kusema kuwa wamemkuta akiwa na risasi 356, magazine 2, msumeno mdogo na mafuta ya kusafishia silaha.

Kufuatia kufanikisha kumkamata kijana huyo kabla ya kutekeleza ujangili Waziri Kigwangalla amesema kuwa wataendelea kutumia mbinu za kisasa zaidi za kiintelinjesia kuthibiti ujangili na kudai kuwa watahakikisha wanakamata majangili kabla ya hawajafanya ujangili.

"Tutaisambaratisha na kuifumua kabisa mitandao ya biashara haramu ya ujangili nchini" alisisitiza Kigwangalla

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )