Saturday, October 14, 2017

Kikwete Akerwa na Watu Wanaopinga Maendeleo


Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amefunguka na kuonyesha kuwa anaumizwa na watu ambao wanapinga maendeleo ya nchi hivyo amemuomba Mungu awaanike watu hao ambao wanapinga maendeleo ili wafahamike.

Ridhiwani Kikwete amesema hayo leo Oktoba 14, 2017 siku ya kilele cha mbio za Mwenge nchini na kumbukumbu ya miaka 18 ya kifo cha mwalimu Nyerere ambao sherehe hizo kitaifa zimefanyika Zanzibar katika uwanja wa Amani.

"Ewe Mwenge mulika wapinga maendeleo, tuwajue..mulika wala rushwa, uwaumbue....Mulika wezi wa mali ya umma...wadhibitiwe...mulika amani yetu, tuiinue. Mjaalie kiongozi wetu Dr.John Magufuli utumishi uliotukuka. Wajaalie na wasaidizi wake kuchapa kazi" aliandika Ridhiwani Kikwete

Aidha Ridhiwani Kikwete amesema kuwa Mwenge wa Uhuru nchini unafaida nyingi sana ikiwepo kuangalia miradi inayofanywa na wananchi na serikali na maendeleo yanayofanyika katika maeneo mbalimbali hasa maeneo ya vijijini. 
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )