Sunday, October 22, 2017

Maagizo Aliyopewa Sugu na Tundu Lissu

Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Joseph Mbilinyi amefunguka na kusema ameagizwa na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuwaambia wana Mbeya pamoja na Watanzania kiujumla kuwa wajiandae.

Joseph Mbilinyi amesema hayo baada ya kumtembelea Tundu Lissu jijini Nairobi nchini Kenya na kusema kutokana na uimara ambao Tundu Lissu anao amewataka Watanzania kujianda.

"Nimemtembelea 'Big hommie', Nairobi hospital. Ameniambia nikawaambie wana Mbeya kuwa alisikia mwitikio wao wa kishindo nilipomtaja kwenye jukwaa la muziki na kuwa mwili wake 'uliovunjwa vunjwa' kwa risasi unazidi kuimarika na atasimama tena. Ameniagiza niwaambie wana Mbeya na Watanzania wote wajiandae, wajiandae, wajiandae" alisema Sugu.

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini juzi walimtembelea Tundu Lissu jijini Nairobi Kenya anapopatiwa matibabu kufuatia kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma Septemba 7, 2017. 
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )