Tuesday, October 17, 2017

Mahakama Kuu Kenya yaondoa zuio la maandamano

Mahakama Kuu nchini Kenya imeondoa kwa muda zuio la maandamano ya muungano wa vyama vya upinzani nchini humo (NASA) katika miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu lililowekwa na Serikali.

Zuio hilo la kufanya maandamano katika miji hiyo ya kibiashara ilitolewa wiki iliyopita na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Kenya, Fredi Matiangi ili kuweza kuondokana na uharibifu ambao ungeweza kujitokeza, lakini zuio hilo limeondolewa baada ofisa mtendaji mkuu wa Nasa, Norman Magaya kufungua kesi mahakamani.

Aidha, Jaji John Mativo ametoa zuio la kukamatwa kwa Magaya kutokana na maandamano ya Nasa hadi kesi yake itakaposikilizwa na kutolewa hukumu.

Hata hivyo, Katika kesi hiyo, Magaya amemfungulia kesi Inspekta Jenerali wa Polisi, Joseph Boinnet, Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka, Keriako Tobiko na Kaimu  Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang’i kwa kuzuia maandamano dhidi ya tume huru ya uchaguzi IEBC.
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )