Friday, October 6, 2017

Mahakama Yamwachia HURU Yusuf Manji Sakata la Madawa ya Kulevya

Mfanya biashara Yusuf Manji leo Oktoba 6 2017 amefutiwa kesi iliyokuwa ikimkabili ya kutumia dawa za kulevya.

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha baada ya upande wa mashtaka na wa utetezi kufunga ushahidi.

Sababu ambayo imepelekea kufutwa kwa kesi hiyo imetajwa kuwa ni upande wa mashtaka ambao ni serikali kushindwa kuthibitisha kosa la mtuhumiwa, Yusuf Manji.

Katika kesi hiyo, Manji anadaiwa kati ya Februari 6 na 9, eneo la Sea View, Upanga wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroine

Mahakama imemuachia huru Manji ikiwa ni siku chache tangu shauri lake jingine la Uhujumu uchumi liondolewe Mahakani hapo na Mkurugenzi wa mashitaka (DPP) ambaye alieleza kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Manji amewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga ambapo alijiuzulu wadhifa huo mapema mwaka huu. Pia Manji alikuwa Diwani wa Kata ya Mbagala kabla ya kuvuliwa nafasi hiyo baada ya kupoteza sifa.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )