Saturday, October 28, 2017

Mbunge akataa milioni 29 alizohongwa na serikali

Mwanamuziki Uganda, ambaye ni Mbunge Kyadondo East , Bobi Wine amekataa fedha milioni 29 za Uganda alizohongwa na serikali ili aweze kukubaliana na mapendekezo ya kufanyia marekebisho kipengele cha katiba na kuondoa ukomo wa miaka 75 kuongoza nchi.

Bobi Wine ameiamuru benki ambayo amewekewa fedha hizo kuzirudisha kwa watu ambao wameziweka na kusema kutokana na taarifa ya mawasiliano wabunge wote wa Uganda 449 wamepewa fedha hizo ili waweze kukubaliana na hoja hiyo na kuoandoa ukomo wa miaka 75 ili kuweza kumpa nafasi tena  Yoweri Kaguta Museveni (73) kugombea nafasi ya Urais tena kwa awamu ya sita 2021.

"Oktoba 24, 2017 Milioni 29 wa Uganda ziliwekwa kwenye Account yangu ya benki, pesa hizo walipewa wabunge wote wa Uganda kwa mujibu wa taarifa rasmi pesa hizo walizopewa wabunge ni ili kukubaliana na pendekezo la kufanyia marekebisho kipengele cha 102 (b) cha Katiba ya Uganda na kuondoa ukomo wa miaka 75 kama sifa ya kusimama kama Rais wa Uganda" alisema Bobi Wine

Bobi Wine aliwapa taarifa watu wa benki yake kuwa wazirudishe hizo fedha zote zilizotumwa kwa mtu ambaye amezituma kwake na kusema amefanya maamuzi hayo kutokana na ukweli kwamba yeye haungi mkono Katiba yao kuchezewa kwa ajili ya mtu mmoja na kusema hawapo tayari kwa mtu kuwa Rais kwa wakati wote ndiyo maana Katiba iliweka ukomo wa miaka. 

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )