Wednesday, October 11, 2017

Mke wa Sheikh Jumuiya ya Uamsho Ambaye mumewe yuko Mahabusu AJINYONGA

Mke wa Sheikh Suleiman Othman mmoja wa wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho wanaoshikiliwa mahabusu Tanzania Bara amejiua kwa kujinyonga.

Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja imesema Rahma Mussa Koki (28) alijiua kwa kujinyonga Jumapili

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Hasina Ramadhan Taufiq amesema watu watano wamehojiwa wakiwemo wazazi wake kuhusu tukio hilo.

Amesema katika mahojiano bado hawajatambua sababu za mwanamke huyo kujinyonga.

“Katika hatua za awali tumesikia alianza kuugua maradhi ya akili na huenda yakawa chanzo cha yeye kuijua,” amesema Taufiq.

Amesema licha ya watu hao kuhojiwa, hakuna wanayemshikilia.

Kamanda Taufiq amesema kazi ya Jeshi hilo ni kuhakikisha wanaendelea na upelelezi na utakapokamilika watatoa taarifa.

Wakati huohuo, Safia Kombo Sheha, mama mzazi wa Rahma amesema kabla ya kifo chake alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya akili na alipatiwa matibabu mara kadhaa.

“Kabla ya kifo chake kama wiki nzima alikuwa akisema nitajinyonga nasi tukawa karibu naye kila wakati kwa kujua ni
mgonjwa. Jumapili asubuhi tulikuwa pamoja ila niliondoka kidogo. Niliporudi nilikuta mlango wa chumbani kwake umefungwa, tulipouvunja tulikuta akiwa amejinyoka kwa kutumia kamba,” amesema.

Safia amesema baada ya ndugu na majirani kufika walibaini alishafariki. Tukio hilo amesema lilitokea saa nne asubuhi, eneo la Kigunda, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Rahma ameacha watoto watatu, wawili wakiwa wa kike.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )