Friday, October 27, 2017

Mume na Mke Wauawa kwa Mapanga Usiku

Mume na mke wameuawa kwa kukatwa mapanga wakiwa wamelala nyumbani kwao.

Wanandoa hao walikuwa na kesi mbili za kugombea ardhi katika baraza la aridhi la Kata ya Hunyari, Tarafa ya Chamriho wilayani Bunda.

Ofisa Tarafa ya Chamriho Boniphace Maiga, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 22, mwaka huu.

Aliwataja waliouawa  kuwa ni Magina   Masengwa (61) na mke wake, Sumaye Sebojimu (58) ambao wote ni wakazi wa kitongoji cha Kiborogota Kijiji cha Mariwanda wilayani Bunda.

Maiga alisema   wanafamilia hao walivamiwa usiku na watu wasiojulikana na wakiwa wamelala na kukatwa mapanga kabla ya wavamizi hao  kutoweka na kuacha maiti za watu hao ndani ya nyumba hiyo.

Maiti hao waligundulika kesho yake asubuhi na mjukuu wao aliyekuwa anakwenda shambani.

“Ofisi yangu ilipokea taarifa ya mauwaji hayo kwamba watu wawili mume na mke wameuawa kwa kukatwa mapanga.

“Kwa hiyo chanzo cha mauaji hayo inasadikika huenda kinatokana na mgogoro wa shamba kwa sababu  walikuwa na kesi mbili katika baraza la ardhi la Kata ya Hunyari,” alisema Maiga.

Alisema   polisi walimkamata   Nyangi Nyabirumo, mkazi wa kijiji hicho kwa mahojiano na anaendelea kushikiliwa Kituo cha Polisi Wilaya ya Bunda.

Maiga alitoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.

Alisema  hali hiyo inaweza kusababisha upande wa pili nao kukasirika na kulipiza kisasi jambo ambalo  ni kinyume cha sheria.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )