Saturday, October 28, 2017

Ofisi za Manji zafungwa, kisa kodi ya Sh300 milioni

Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji ameendelea kuingia matatani baada ya Kampuni ya Udalali ya Yono kuzifunga ofisi zake zilizopo Barabara ya Pugu.

Yono wamezifunga ofisi na maghala ya Manji ambaye alikuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga akituhumiwa kudaiwa kodi ya zaidi ya Sh300 milioni na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Yono, Scholastika Kevela jana Ijumaa  alisema, ‘’ni kweli tumezifunga ofisi za Manji zilizopo eneo la Pugu, anadaiwa fedha nyingi za kodi na TRA.”

Alipoulizwa kipi kitafuata baada ya kuzifunga, Kevela alisema, ‘’sisi utaratibu wetu ni kwamba tukizifunga huwa tunatoa siku 14 mhusika akalipe na baada ya hapo sasa tunasubiri maelekezo kutoka kwa TRA.”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )