Monday, October 2, 2017

Rais Magufuli Hatakuwa Mgeni Rasmi Kongamano la Kumbukizi ya Mwl. Nyerere

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli hatakuwa mgeni rasmi katika kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kama inavyotangazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Tarehe 11 Oktoba, 2017 ambayo inatangazwa kuwa ndio siku ya kufanyika kwa kongamano hilo, Mhe. Rais atakuwa na majukumu mengine ya Kitaifa kulingana na ratiba yake ya kazi.

Taasisi mbalimbali za umma na zisizo za umma zinazomualika Mhe. Rais katika shughuli zao zinakumbushwa kutokutangaza ushiriki wa Mhe. Rais katika shughuli zao mpaka zipate uthibitisho kutoka ofisi ya Rais.

Tafadhali tuzingatie utaratibu huu.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )