Monday, October 23, 2017

Rais Magufuli leo anatarajia kuwatunuku vyeti wote waliofanikisha kufikiwa makubaliano kati ya serikali na Kampuni ya Madini ya Barrick

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Oktoba, 2017 atawatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia na baadaye kufanya mazungumzo na kampuni ya Barrick Gold.

Tanzania na Barrick Gold Corporation zilifikia makubaliano tarehe 19 Oktoba, 2017 na kutiliana saini mkataba wa kutekeleza mwelekeo mpya wa namna kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya dhahabu yanayochimbwa katika migodi yake hapa nchini, pamoja na kulipa Dola za Marekani Milioni 300 za kuonesha nia njema ya kufidia madai ya upotevu wa mapato yaliyotokana na biashara hiyo.

Tukio hili litafanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 5:00 asubuhi na kurushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao mbalimbali.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

23 Oktoba, 2017
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )