Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, October 8, 2017

Serikali yabadili mfumo wa ulipaji mishahara kwa watumishi kubana matumizi

adv1
Ili kupunguza gharama za uendeshaji, Serikali imetangaza kuachana na matumizi ya karatasi kutoa nakala za malipo ya mshahara (salary slip) kwa watumishi wa umma.

Badala yake, Serikali sasa itaanza kutumia mfumo wa kielektroniki.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili na Wizara ya Fedha na Mipango, imesema watumishi wa umma wataanza kutumia mfumo huo kwenye masuala yao yote ya kiutendaji ikiwemo kukamilisha mahitaji ya taasisi za fedha watakapokuwa wakihitaji mkopo au wanaposhughulikia mafao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Taarifa hiyo imesema hata wastaafu watapaswa kufuata utaratibu huo mpya pamoja na wadau wengine wanaoshirikiana na wafanyakazi wa umma yakiwemo mashirika ya bima.

Ili kupata nakala hiyo, maelekezo yanasema kila mtumishi au mstaafu serikalini atahitaji kujisajili.

Taarifa imesema kutokana na gharama kubwa za uchapishaji, usambazaji na usumbufu wa kuzitafuta nakala hizo, wizara imeandaa mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa hati za malipo ya mshahara ujulikanao government salary slip self service.

Imeelezwa utaratibu wa kujisajili na kuutumia mfumo huo unatolewa na waajiri.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )