Saturday, October 14, 2017

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kuahirishwa Kwa Mnada Wa Tanzanite

Wizara ya Madini inatoa taarifa kwa umma kuwa  Mnada wa Madini ya Tanzanite uliokuwa ufanyike katika mji mdogo wa Mererani Wilayani Simanjiro mkoani Manyara kuanzia tarehe 12 hadi 15 Oktoba, 2017, umeahirishwa hadi hapo utakapotangazwa tena.

Sababu za kuahirishwa kwa mnada huo ni kuridhia maombi ya wadau wa mnada ambao waliomba kupata muda zaidi wa maandalizi ili wapate fursa ya kushiriki kwa wingi. 

Aidha, uongozi wa Wizara na Mkoa wa Manyara watapata muda zaidi wa kuandaa mazingira salama na bora zaidi ya kufanyia mnada huo katika mji wa Mererani.

Hivyo, Wizara ya Madini inawaomba radhi wadau wote wa Sekta hii ndogo ya madini ya vito hususan Tanzanite ambao wameathirika kwa namna moja au nyingine kutokana na kuahirishwa ghafla kwa mnada huu.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )