Friday, October 20, 2017

Uamuzi wa pingamizi kesi ya Mdee, Bulaya Oktoba 30

Mahakama Kuu Oktoba 30,2017  itatoa uamuzi wa pingamizi zilizowasilishwa na upande wa Serikali katika maombi ya wabunge wa Chadema waliosimamishwa kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge kwa kosa ya kudharau kiti cha Spika.

Wabunge hao waliosimamishwa katika Bunge la bajeti Juni, 2017 ni Halima Mdee wa Kawe na Ester Bulaya wa Bunda Mjini.

Mdee na Bulaya wamefungua mashtaka katika Mahakama Kuu wakidai uamuzi huo umekiuka Kanuni za Bunge na Katiba.

Katika kesi hiyo jana  Alhamisi Oktoba 19,2017 mawakili wa wabunge hao, Jeremia Mtobesya na Fred Kalonga waliiomba Mahakama iwaelekeze Spika wa Bunge au Katibu Bunge wawapatie taarifa walizoomba na kutoa ruhusa ya kuzitumia.

Wakili Mkuu wa Serikali, Angaza Mwipopo aliyewasilisha pingamizi kwa hati ya kiapo alidai wabunge hao hawakutumia fursa zingine walizonazo kabla ya kufungua shtaka hilo mahakamani.

Jaji Awadhi Mohamed aliyesikiliza pingamizi hizo ameahirisha maombi hayo akisema uamuzi atautoa Oktoba 30,2017.
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )