Friday, November 3, 2017

Bodi ya mikopo Yawatoa Hofu Wanafunzi


Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu nchini (HESLB) imewatoa hofu wanafunzi waliokosa mikopo kwakuwa ipo katika hatua za mwisho kutoa majina ya awamu ya tatu.

Kauli hiyo imekuja ikiwa leo   ni siku ya mwisho iliyotolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ya kuitaka bodi hiyo kuhakikisha kila mwanafunzi mwenye sifa anapewa mkopo.

Akizungumza leo Novemba 3,Meneja Mawasiliano wa bodi hiyo, Omega Ngole amesema agizo hilo linaendelea kutekelezwa na kwamba hadi kufikia kesho  kila mwanafunzi mwenye sifa atapata mkopo.

Amesema kwa wale watakaokosa mkopo wanaweza kukata rufaa kupitia bodi hiyo ili kupitia upya taarifa zao.

“Maelekezo hayo yote yanatekelezwa na tutakamilisha leo na tutatoa taarifa ya kuhusu utekelezaji wake wiki ijayo,” amesema

Katika mwaka wa masomo wa 2017/18 Serikali imetenga bajeti ya Sh427 bilioni kwaajili ya mikopo ambapo wanafunzi 30,000 wa mwaka wa kwanza watanufaika na fungu hilo.

Hadi sasa Jumla ya wanafunzi 21,677 maombi yao yamekubaliwa ikiwa ni awamu mbili zilizotolewa na bodi hiyo ambapo awamu ya kwanza ilitoa majina 10,196 na ya pili 11,481.

Meneja huyo amesema kwa wale waliodahiliwa kwenye vyuo walivyothibitisha kupitia Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) tayari fedha zimeanza kutumwa kwenye vyuo husika.

“Mwanafunzi akipangiwa mkopo halafu asipoliridhika, akaona uhitaji wake ni mkubwa kuliko kiwango alichokipata kuna nafasi ya kukata rufaa ambayo itaanza wiki ijayo,”amesema.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )