Tuesday, November 28, 2017

BREAKING NEWS: Makamu wa Rais amtembelea Tundu Lissu Nairobi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea ma kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki kupitia CHADEMA, Tundu Lissu anayepatiwa matibabu jijini Nairobi Kenya.

Makamu wa Rais ambaye alikwenda Kenya mapema leo asubuhi kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa aliyekuwa Rais Mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta, alifika hospitalinia hapo mapema leo jioni majira ya saa 11.

Samia Suluhu alifika kumjulia hali Tundu Lissu akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana pamoja na maofisa wengine.

Makamu wa Rais alikuwa njiani kurejea nchini Tanzania wakati alipofika hospitalini hapo.

Tundu Lissu amelazwa katika Hospitali ya Nairobi tangu Septemba 7 baada ya kujeruhiwa kwa kushambuliwa kwa risasi akiwa mjini Dodoma eneo la Area D.

Kwa mujibu wa Spika wa Bunge, Job Ndugai, Lissu alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30 ambapo risasi 5 tu ndizo zilimpata katika maeneo ya mkononi, tumboni na mguuni.

Makamu wa Rais amekuwa kiongozi mwandamizi wa serikali wa kwanza kumtembelea Lissu hospitalini hapo. Wengi ambao wamekuwa wakimtembelea ni wabunge wenzake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )