Thursday, November 2, 2017

Hausigeli: Nilitega Limbwata Kwa Baba Mwenye Nyumba Likamnasa Mama Mwenye Nyumba

Jina  langu  ninaitwa  Vumy.
Nilikuwa  dada wa  kazi ( Hausigeli ) nikamtamani kimapenzi  baba  mwenye nyumba kwa  sababu  alikuwa  na  pesa  na  mali  nyingi sana. Nilijua  nikiwa  nae kimapenzi  basi  shida  zangu  zote  zitaisha.
 
Nikaenda  kuomba ushauri kwa  rafiki  mmoja  ambae  akanielekeza  kwa  mganga  mmoja  wa  kienyeji  ili  anipe  dawa  niweze  kumkamata  kichawi  baba  mwenye  nyumba.
Rafiki  yangu  aliniambia mganga  huyo  ni  hatari  sana  kwenye  dawa  za  mapenzi  na  kwamba  endapo  nitafanikiwa  kuonana  nae  basi  huyo  mwanaume nitamkamata  na  atafanya  kila  kitu  ninacho  kitaka.

Nilipo enda  kwa  mganga  nikapewa  dawa  ya  kumuwekea  baba  mwenye  nyumba  kwenye  chakula  anachokula .
 
Mganga  akanipa  sharti  moja  akaniambia, nihakikishe  hicho  chakula  hali  mtu mwingine  yoyote  yule  isipokuwa  baba  mwenye  nyumba  na  ikitokea  nikivunja  sharti  hilo  nitapata  madhara makubwa  sana   ambayo  hakutaka  kuyaweka  wazi.

Hilo  lilikuwa  sharti  rahisi  sana  Kwangu, kwa  sababu  mara  nyingi  baba  mwenye  nyumba  huwa  anarudi  usiku  na  huwa anakula  chakula  chake  peke yake  na  mara  nyingi  huwa  anamkuta  mke  wake  ameshakula  na  amelala.
 
Siku  hiyo  usiku  mama  mwenye  nyumba  akasema  hali  chakula  kigumu, atakunywa  maziwa  fresh  tu  ya  moto.
Nikamtayarishia  kama  alivyo  agiza  wakati  huo  huo  baba  mwenye  nyumba  nikamuandalia  ugali  na  nyama  na  maziwa  mtindi  na  kuweka  dawa niliyopewa  na  mganga  kwenye  nyama  ili  baba  mwenye  nyumba  akila  hiyo dawa  anase  na  anipende.

Sijui  kitu  gani  kilimvutia? Sijui ni  harufu  ya  chaklula  au  alipatwa  na  njaa  ghafla, mama  mwenye  nyumba  akaniambia  amekipenda  hicho  chakula,anaomba  nimpe  ale  halafu  baba mwenye  nyumba  nimuandalie  chakula  kingine.
 
Nilichanganyikiwa  lakini  sikuwa  na  jinsi  zaidi  ya  kumpa  chakula  nilicho  kiandaa  kwa  baba  mwenye  nyumba  ambacho  nilikuwa  nimekiwekea  limbwata  ili  baba  mwenye  nyumba  anase.
 
Baada  ya  kumpa  mama  mwenye  nyumba  chakula  nikaenda  chooni  na  kumpigia  simu  mganga  kumwambia  kilicho  tokea.
 
Nilivyo mpigia  simu mganga  akaniambia  kwa  ukali  kwamba   alinionya  tangu  mwanzo  niwe  makini  na  hiyo  dawa   na  kuniambia nisubiri  kitakacho  nitokea.

Kesho  yake  asubuhi  yule  mama  mwenye  nyumba akaanza  kuonyesha upendo  na  mapenzi  ya  hali  ya  juu  sana  Kwangu kiasi  nikaogopa.  Mapenzi ya  mama  mwenye  nyumba  Kwangju  yalikuwa  yanaongezeka  saa  hadi  saa  kiasi  akawa  anafanya  vitu  ambavyo  mimi ndo  natakiwa  kuvifanya  kama  vile  kuosha  vyombo, kufua  nguo, kupika  nakadhalika.
 
Baada  ya  kama  siku  tatu  hivi , uzalendo  ukamshinda  akaamua  kunitamkia  laivu  kwamba  ananipenda sana   na  kwamba  anataka  tuanzishe uhusiano  wa  kimapenzi.
 
Nilimwambia  siwezi  kufanya  hivyo, sijawahi  kufanya  hivyo  wala  sitarajii  kuwa  katika  mahusiano  na  mwanamke  mwenzangu  lakini  wala  hakuweza  kunielewa.
 
Akaniahidi  vitu  vingi sana.Kunisomesha  chuo, kumlea na  kumsomesha  mtoto  wangu,kunijengea nyumba,  kuninunulia  gari,  mashamba, viwanja, kunifungulia  akaunti  benki  na  biashara.
 
Vyote  nikakataa  na kumwambia  siwezi  kuwa  katika  mahusiano  ya  kimapenzi na  mwanamke  mwenzangu.
 
Nilivyo ona  usumbufu  umezidi  nikaamua kuondoka  na  kurudi  nyumbani  kwetu  kijijini  Kondoa, lakini  kwa  kuwa  alikuwa  anajua natoka  sehemu  gani  Kondoa, na  namba  za  simu  za  mama  angu  alikuwa  nazo, akanifuata  hadi  Kondoa  na  kuniomba  nirudi  kufanya  kazi  kwake.
 
Akanipa  hela  nyingi  na mama  angu  pia  akampa  hela. Mimi  nikamwambia  kuna  mambo  nayamalizia  kijijini  Kondoa  yeye  arudi  zake  dar  nitamfuata  baada ya  wiki  moja, akakubali  kwa  shingo  upande.
 
Alivyo ondoka  kijijini  nikamwambia  mama  angu siwezi  kwenda  kwa  huyo  mwanamke  kwa  sababu  nimeambiwa  ni  freemason.  Sikutaka  mama  angu  ajue  kitu  gani  kinaendelea.
 
Ilivyo  pita  wiki  moja  sijaenda  akaanza  kusumbua  kwa  simu, nikawa  sipokei.
Akaanza  kumsumbua  mama  angu  na  kumuomba  anibembeleze  nirudi  kufanya  kazi  kwake.
 
Katika  kumlainisha  mama  angu  akawa  anamtumia  hela  nyingi  tu mpaka  mama  angu  akahamia  upande  wa  huyo  mwanamke  na  kunishawishi  niende  kufanya  nae  kazi.
Kama  hiyo  haitoshi   amemjengea  nyumba  mama  angu  kijijini  na  huwa  anakuja  kijijini  kwetu  linapotokea  tatizo  lolote  la  kifamilia  au  sherehe.
 
Yote  hayo  anayajua  kwa sababu  anawasiliana  sana  na  mama angu.
Hiyo  ilikuwa  mwaka  2015  mwishoni  lakini mpaka  sasa  hivi  bado  ananisumbua  na  nimeshamwambia  kuwa  sipo  tayari  kufanya  upuuzi  huo.
 
Yupo  kama  aliye  changanyikiwa  au  aliye  pagawa  na  pepo.
Amegombana  na  kutengana  na  mume  wake  kwa  sababu  yangu .
Kuna  kipindi  alikuwa  ananipigia  simu  kunibembeleza  niwe  nae  mbele  ya  mume  wake.
 
Mume  wake  alipofariki  ndugu  walimzuia  kushiriki  kwenye  mazishi  kwa kumtuhumu  kusababisha  kifo  cha  mume  wake.
Lakini  bado  ananin’gan’ania  tu  licha  ya  kumwambia  mimi  sipo  tayari  kufanya  anavyo  taka  yeye.
 
Kuna  kipindi  nilirudi  kijijini  kulima  ufuta  na  kukaa  huko  kwa  miezi  mitatu  na  yeye  akaja  kukaa  kijijini  na  kuchukua  mashamba  alime  ufuta  lakini lengo  lilikuwa  kuwa  karibu na  mimi.
 
Katika  kipindi  chote  hicho  usumbufu  ambao  amekuwa  akinipa  ni  mkubwa  mno.
Amekuwa  kama  zezeta  au  mtu  aliye  pagawa  hivi.
Nimejaribu  kila  njia  ya  kumkwepa  huyu  mama  lakini  imeshindikana.  .
 
Nimemwambia si awatafute wanawake  wenye  tabia  hizo  anasema  ananitaka  mimi  na sio  mtu  mwingine  yoyote  yule.
 
Nimejaribu  kwenda  kwa  mganga  alio  nipa  hiyo  dawa  na  kumwambia  anitenganishe  na  huyu mwanamke  amekataa  kata  kata  anasema  huo  sio  utaratibu  wake  wa  kazi  na  kwamba  uchawi  huo ni  wa  maisha na  hauwezi  kubatilishwa  kwa  namna  yoyote  ile hadi  naingia kaburini.
 
Utaisha  nguvu  pindi  mmoja  wetu  atakapo  itwa  na  Mungu  kwa  hiyo  nivumilie  tu  kwa  sababu  mimi  ndio  nilifanya  uzembe.

Siwezi kuendelea  kuishi  katika  hali  ya  usumbufu  mkubwa  kiasi  hiki.
 
Tena mganga  kaniambia  halafu  nina  bahati  kwa  sababu  kuna  wengine  huwa  wanafanyaga  uzembe  dawa  anakula  baba  mzazi  au  mtoto  au  kwa  wanaume  dawa  anakula  mama  mzazi , mtoto  au  dada   ambao  wengi  wao  huishia  kukimbia  nchi  au hata  kujaribu  kujiua.
 
Kwa  hivyo  nishukuru walau  nina  bahati.
Nimejaribu  kwenda  kwa  waganga  na  waganga  lakini  wapi.
Imeshindikana  kumzuia  mwanamke  huyu  asiendelee  kunin’gan’gania.
 
Nimejaribu  kuombewa  kote  imeshindikana.
SASA  NDUGU  ZANGU. NINAOMBA  MSAADA  WENU. NITUMIE  NJIA  GANI ILI  KUMFUNGA  HUYU MAMA  ASIENDELEE   KUNIFUATA  FUATA  NA  KUNIGANDA ?

AU  KUNA  NJIA  YOYOTE  INAYO WEZA  KUTUMIKA KUMZINDUA  HUYU  MWANAMKE  NA  KUMFANYA  ARUDI  KATIKA  HALI  YAKE  YA  KAWAIDA ?  YAANI  AJITAMBUE  KWA  SABABU  NAONA  ANAE  ANYA  HIVYO  SIO  YEYE  ILA  NI  HUO  UCHAWI  NILIO MLISHA  KWA  BAHATI  MBAYA ..
 
JAMANI  KAMA  KUNA  MTUMISHI  YOYOTE  WA  MUNGU   ANADHANI  ANAWEZA  WALAU  KUMUOMBEA  HUYO  MAMA  ILI  ARUDI  KATIKA  HALI  YAKE  YA  KAWAIDA, MIMI  NIPO  TAYARI  KUMUELEKEZA MAHALI  ANAPOISHI  HUYO  MAMA AWEZE  KUFANYA  UTARATIBU  WA  KWENDA KUMUOMBEA  NA  KUMRUDISHA  KATIKA  HALI  YAKE  YA  KAWAIDA
NA  KAMA  KUNA  MTU  ANAWEZA KUFANYA  MAOMBI  YA  KUMZUIA HUYO  MAMA  ASIENDELEE  KUNIFUATILIA  TAFADHALI  SANA  NAOMBA AWASILIANE  NAMI.
 
HATA  KAMA  UNAJUA MAHALI  NINAPO WEZA  KUPATA MSAADA  TAFADHALI  NIFAHAMISHE.

Niandikie  kupitia  barua  pepe  yangu :
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )