Tuesday, November 7, 2017

Jeshi la Polisi Laichukua Simu ya Zitto Kabwe

Simu ya mkononi ya Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe imechukuliwa na vyombo vya dola kwa uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini, anatuhumiwa kwa makosa ya sheria ya mitandao na takwimu.

Mbunge huyo leo Jumanne Novemba 7,2017 amefika kitengo cha uhalifu wa makosa ya kifedha kilichopo Kamata, Kariakoo jijini Dar es Salaam kujua hatima yake.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi hizo, Zitto amesema, ''Nimeambiwa nirudi hapa Novemba 21,2017 lakini wamechukua simu yangu wanadai niliitumia kusambaza taarifa za takwimu nami nimewaachia kwa kuwa wana haki hiyo."

Amesema, "Kwa sasa sitapatikana, watu waliokuwa wananitafuta hawatanipata, kwa hiyo ndio hivyo wameamua wao lakini niwahakikishie tu kuwa mawasiliano niliyokuwa nayafanya yanalinda uhuru wangu wa Kikatiba."

Zitto amesema kabla ya kuwapatia simu walijadiliana kuhusu uamuzi huo lakini mwisho akaona awaachie wafanye wanavyotaka wao.

Amesema upekuzi pia utafanyika katika ofisi za ACT-Wazalendo na haijajulikana utafanyika lini.
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )