Tuesday, November 14, 2017

Kitabala: Lulu Anaweza Kupata Dhamana Akisubiri Rufaa Kusikilizwa

Wakili wa Elizabeth Michael ‘Lulu’, Peter Kibatala, kufuatia hukumu ya miaka miwili dhidi ya Lulu jana, ametoa ufafanuzi kupitia akaunti yake ya Instagrame kuhusu kitakachofuata alipoulizwa maswali na watu wengi ambapo alitumia fursa hiyo kuwafafanulia sheria inavyosema kuhusu nini kinafuata.

Majibu yake kwa maswali hayo ni yafuatayo:
  1. Amesema kuwa hakuna hukumu tofauti inayoweza kutolewa kabla mhukukiwa hajatumikia theluthi ya kufungo chake ambacho kwa Lulu itakuwa ni kuanzia miezi  mitano.
  2.  Ndani ya hiyo miezi mitano dhamana inaweza kuombwa wakati wakisubiria rufaaa ianze kusikilizwa.  Kwa maana hiyo anaweza kutoka kwa dhamana muda wowote mahakama ikmpatia dhamana.
  3. Huwezi kuacha kijana wa miaka 22 mwenye maisha marefu mbele yake ahukumiwe kwa uhalifu kwa sababu ya suala la muda, kwani itaharibu maisha yake ya mbele. Kwa hiyo rufaa imelenga katika kuondoa tatizo hilo.
  4.  Kukata rufaaa na kuomba dhamana  na kufanya kazi za jamii vinaweza kufanyika kwa wakati mmoja wakati suala hili likisubiriwa kusikilizwa na mahakama ya rufaa.
==>Huu ndo Ujumbe wa Kitabala katika Instagram yake

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )