Monday, November 27, 2017

Magdalena Sakaya: Sipo Tayari Kuhama CUF na Kama Kitafutwa Basi Ntastaafu Siasa

Naibu Katibu wa CUF Tanzania Bara, Magdalena Sakaya  amedai hayuko tayari kuondoka Chama cha Wananchi CUF na kwenda katika vyama vingine hata kama chama chake kina mgogoro na iwapo na ikitokea Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ikiamua kukifuta chama hicho yeye atastafu siasa

Akifanya mahojiano maalumu na Nipashe, Sakaya amesema kwamba Mgogoro unaoendelea ndani ya chama chao ni wa Kikatiba na unafahamika kwa msajili wa vyama na kuongeza kama ikitokea kwamba CUF inafutwa basi yeye atastaafu siasa na siyo kuhama chama.

"Kwanza naamini CUF haiwezi kufutwa. Yaani hilo halipo pamoja na changamoto ya mgogoro iliyopo. CUF ina misingi yake na mgogoro uliopo ndani yake ni wa kikatiba. Kwa hiyo, mimi nikiamua kwamba sasa sitaki kuendelea kuwapo CUF, ninaacha siasa. Ninaendelea na mambo yangu mengine, eeeh" Sakaya

"Kwanza mimi sijawahi kuwa na kadi ya CUF pekee. Nakumbuka wakati tunaripoti Shule yaSekondari ya Wasichana Kibosho (mwaka 1986) tuligawiwa kadi za kijani (CCM) wakati ule nchini kulikuwa na chama kimoja. Baadaye nikiwa na akili yangu timamu kadi niliyoichukua ni ya CUF ambayo niliichukua mwaka 1995 na ninayo mpaka leo na nitaendelea kuwa nayo. .
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )