Loading...

Thursday, November 23, 2017

Masharti Magumu ya mnada yaliyowekwa na Yono Aution Mart

Kampuni ya Udalali ya Yono imetangaza kuwa kesho, Novemba 24, 2017 itarudia upya mnada wa nyumba mbili za kifahari za mfanyabiashara Said Lugumi zilizoshindikana kuuzwa baada ya Dr. Louis Shika kuzinunua na kushindwa kuzilipia.

Nyumba zilizotajwa kurudiwa kuuzwa katika mnada ni Plot. No 47, iliyopo Mbweni JKT,  na nyingine iliyopo Upanga

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Mart, Scholastica Kevela ameeeleza kuwa kwa sasa kampuni ya Yono imeweka masharti magumu ili kuhakikisha kwamba hakuna atakayeibuka kuuharibu mnada huo.

“Niwakaribishe wateja ndani na nje ya nchi kuja kujinunulia nyumba zile kwa maana ujenzi ni mgumu..” amesema.

Aidha Bi Scholastica Kevela amewaonya wale wote wenye nia ya kuuharibu mnada huo kutofanya hivyo kwani hawatavumiliwa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

“Niseme kwamba mchezo ule tuliochezewa mara ya mwisho hautarudiwa tena. Kwa sasa hivi tumekuja na masharti magumu kwamba washiriki wote wawe aware na wanielewe,” amesema Bi. Kevela.

Masharti yaliyowekwa katika minada hiyo ni kwamba mshiriki atapaswa kujiandikisha kwenye kitabu maalum cha washiriki wa minada, baada yahapo atajaziwa ‘commitment form’ (fomu maalumu ya kushiriki mnada).

Baada ya hayo, vitambulisho vya mshiriki ikiwemo hati ya kusafiria (passport), leseni ya udereva na kitambulisho cha mpiga kura vitachukuliwa na kampuni.

Kila mshiriki halali atapaswa kulipa kiasi cha shilingi milioni 2 kupitia akaunti ya Yono ili kuthibitisha kuwa ana lengo la kushiriki. Kwa atakayeshinda mnada, fedha hizo (sh. 2 milioni) zitatumika kama sehemu ya malipo. Kwa ambao watakosa basi fedha zao zitarudishwa hapo hapo.

Kwa watakaoshiriki kuharibu mnada, hawatorudishiwa fedha hizo na watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwa mshindi atakayepata nyumba atatakiwa kulipa hapohapo 25% ya gharama yote ya nyumba na 75% ya gharama inayobaki atapaswa kulipa ndani ya muda wa siku 14.

Yono Auction Mart wametoa onyo kubwa kwa watakaohusika kwa namna yoyote kuharibu minada hiyo kuwa watakamatwa na kufunguliwa kesi mahakamani kwa kuwa na nia ovu ya kukwamiha ukusanyaji wa kodi ya serikali.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )