Saturday, November 18, 2017

Serikali Ya Burundi Yanuia Kuwarejesha Wananchi Wake Waliokimbilia Tanzania

Serikali ya Jamhuri ya Burundi imesema ipo tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali katika kuhakikisha zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi waliopo nchini Tanzania wanarejea nchini Burundi kwa haraka ili wakaijenge nchi yao.

Haya yamezungumza na Waziri wa mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo kutoka Jamhuri ya Burundi Mhe. Pascal Barandagiye, alipozuru katika kambi za Nyarugusu, Nduta na Mtendeli kutoa ujumbe wa kuwaasa kurejea wakimbizi nchini kwao Burundi.

Tangu zoezi la urejeaji wa wakimbizi lilipoanza mwezi septemba 2017 kwa awamu ya kwanza jumla ya wakimbizi 8347 wameshasaidiwa kurejea nchini kwao Burundi sawa na asilimia 100.3 ya lengo ya urejeshwaji kwa awamu ya kwanza.

Aidha, mwanzoni mwa mwezi Novemba wakimbizi wapatao 33,948 walijiandikisha kurejea nchini kwao Burundi lakini kutokana na kasi ndogo na taratibu ndefu zinazofanywa na Shirika la kuhudumia wakimbizi Duniani UNHCR wakimbizi waliojiandikisha wameanza kusitisha nia yao ya kurejea kwani hawaoni jitihada zinazofanywa kuwarudisha, ambapo jumla ya wakimbizi 735 kati ya 33948 wamesitisha nia yao ya kureja kwa hiari.

Hali hii inatajwa na viongozi wa Burundi kuwa inachelewesha zoezi kwani wakimbizi wanaorejeshwa kwa mujibu wa mpango wa urejeaji ni ndogo. Mhe. Pascal Barandagiye amesema serikali ya yake ipo tayari kutoa magari kwaajili ya kuwasafirishwa wakimbizi kurudi nchi mwao, pamoja na kuwapa huduma muhimu za kibinadamu.

 “zoezi la urejeshaji wa Wakimbizi kwa hiari linaenda polepole mno tofauti na matarajio, shirika la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR linaenda kwa kasi ndogo tofauti na ilivyotarajiwa, hivyo kutokana na zoezi hilonkuenda taratibu Serikali ya Burundi ipo tayari kutoa magari, fedha na huduma nyingine za kibinadamu ili kusaidia kuweza kuharakisha zoezi la kurejesha wakimbizi waliojiandikisha kurejea kwa hiari nchini Burundi” alisisitiza Barandagiye.

Akiongea katika nyakati tofauti tofuti katika kambi za nyarugusu, nduta na mtendeli, amewahakikishia wananchi wa  kuwa Amani nchini mwao ipo ya kutosha hakuna vurugu na serikali ya Burundi inawahitaji ili warejee kuenga taifa lao hakuna haja ya kuendelea kubaki makambini.

Wakimbizi wakiongea kwa nyakati tofauti wamemhakikishia kuwa bado wanapenda nchi yao Burundi, na wanatamani kurejea Burundi, lakini changamoto inayowakabili hadi kukata tamaa ya kurudi ni taratibu ndefu zinazowachelewesha kurejeshwa mara tu baada ya kujiandikisha

 Akiongea kwa niaba ya Wakimbizi walioko kambi ya Nduta Bw. Suleima Hamisi (65) ambaye amekuwa Mkimbizi mara Sita kwa nyakati tofauti tangu mwaka 1972 alisema “ Sisi tulishajiandikisha Zaidi ya miezi mine sasa ili tuweze kurejeshwa cha kushangaza hadi sasa badotupo makambi”  ameiomba serikali ya Burundi na Tanzania na Shirika la kuhudumia wakimbizi wakae na kuzungumza kwa pamoja juu ya mustakabali wa kuwarejesha haraka wenye nia ya kurudi Burundi.

Akitoa taarifa kwa Waziri wa mambo ya ndani na mafunzo ya uzalendo wa Burundi na Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Jamuhuri ya Muungani wa Tanzania, Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu ikiyopo Wilayani Kasulu alisema kumekuwa na mwitikio Mkubwa wa wakimbizi wanao jiandikisha kurejea kwa hiari nchini Burundi lakini changamoto imekuwa taratibu ndefu zinazochelewesha kurejea kwao zinawafanya baadhi yao kuahirisha kurejea kutokana na kusubiri kwa muda murefu.

Serikali ya Burundi pia imedai Shirika la kuhudumia wakimbizi Dunia UNHCR linatakiwa kubadilisha utaratibu wa kuwapatia au kuwagawia vyakula na pesa wakimbizi wanapokuwa wanarejea wameomba zoezi hilo lifanyike wakati tayari wakimbizi wakishapatiwa nyumba na maeneo yao ya makazi kuepusha kukaa kwa muda mrefu kwenye vituo vya kuwapokelea.

Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema serikali ya Tanzania itahakikisha wakimbizi waliopo nchi wanahifadhiwa kwa mujibu wa makubaliano ya taratibu za kimataifa na wale wanaopenda kurejea kwa hiari itashirikiana na UNHCR,  nchi ya Burundi ili kufanikisha zoezi hilo. Hatua ya kuwarejesha wakimbizi katika nchi yao ya asili ni moja kati ya suluhisho la kudumu la ukimbizi kwa mujibu wa sharia ya kimataifa ya wakimbizi ya mwaka 1951 na Sheria ya Wakimbizi ya Tanzania yam waka 1998 kifungu Na. 3

Zoezi la kurejea kwa wakimbizi nchini mwao waliopo Tanzania lilianza kuratibiwa mara tu baada ya tamko la viongozi rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunzinza walipo kutana Mwezi Julai 20, 2017 na kutamka kuwa wakimbizi waliopo Katika Makambi nchi Tanzania warejee nchini kwao kwani Burundi kuna amani ya kutosha.

Hadi sasa idadi ya wakimbizi walioko katika Mkoa wa Kigoma ni 210,005 na waomba hifadhi 26,410, kati ya hao 95,243 wapo kambi ya Nduta, 48147 kambi ya Mtendeli na 66615 Nyarugusu, aidha waombahifadhi wote wapo katika kambi ya nduta.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )