Thursday, November 2, 2017

Tamisemi yasitisha ajira mpya za afya

Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesitisha ajira mpya za kada ya afya zilizoombwa kwa kipindi cha Agosti mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa Oktoba 31 na Tamisemi ikieleza kusitisha ajira hizo kwa walioitwa kazini.

Taarifa hiyo iliwataarifu waajiri na waombaji wote wa nafasi za ajira za kada za afya kuwa imesitisha zoezi hilo kwa muda mfupi ili kukamilisha taratibu za ajira.

“Tafadhali rejeeni tangazo letu lenye Kumb. Na CD. 162/355/01 la tarehe 30 Oktoba, 2017 lililowataarifu waombaji wa kazi wa nafasi mbalimbali za kada za afya walioomba kazi kuanzia 25/07 - 30/08/2017,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imethibitishwa kutolewa na Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Zainabu Chaula ambaye alisema  kuwa ni kweli wamesitisha kwa muda kwa sababu za kiufundi na halihusiani na madaktari wa Kenya.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )