Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, November 29, 2017

TANESCO Wataja Chanzo cha Kukatika kwa Umeme Dar, Pwani

adv1
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa taarifa kwa wateja katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuwa baadhi ya maeneo hayana umeme kutokana na hitilafu iliyojitokeza.

Taarifa ya Tanesco imesema baadhi ya maeneo ya mikoa hiyo hayana umeme kuanzia saa 3:20 asubuhi ya leo Jumatano Novemba 29,2017 kutokana na mashine namba tatu ya kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia kituo cha Ubungo II kupata hitilafu.

“Mafundi wa shirika wanaendelea na jitihada za kutatua hitilafu hiyo kwa haraka ili kurejesha umeme katika hali yake ya kawaida,” imesema taarifa ya Tanesco.

Shirika hilo limesema litaendelea kutoa taarifa za maendeleo ya kazi hiyo.

Pia, Tanesco imetoa tahadhari kwa wananchi kutosogelea, kushika wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Uongozi wa shirika hilo umewaomba radhi wateja kwa usumbufu uliojitokeza.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )