Wednesday, November 1, 2017

Tundu Lissu Amkaribisha Nyalandu......Asema Hatua Aliyoichukua Kujiondoa CCM ni ya Kijasiri

Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu amempongeza aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki(CCM), Lazaro Nyalandu kwa kupata ujasiri wa kuchukua hatua kubwa ambayo hata wabunge wengi waliopo ndani ya CCM wanashindwa kuichukua.

Lissu ambaye yuko kwenye matibabu jijini Nairobi  amempongeza Nyalandu kwa kuwa ni alikuwa mbunge jirani yake na kwa ujasiri wa kufanya hivyo.

Mbali na kumpongeza Nyalandu pia Lissu amezungumzia  uchaguzi wa madiwani katika kata 43 akieleza kuwa kuwapa CCM kura katika kata hizo ni sawa na kukubaliana na yanayoendelea nchini.

“Kuwapa CCM kura sasa hivi ni sawa na kuwapa CCM mamlaka ya kutapanya mali zetu kama wanavyotaka,”amesema Lissu leo Jumanne akiwa jijini Nairobi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )