Thursday, November 9, 2017

Yono yaifunga Hoteli ya Blue Pearl Kwa Kudaiwa Kodi Bilioni 5.7

Kampuni ya Udalali ya Yono imeifunga Hotel ya Blue Pearl  kwa kudaiwa kodi na Ubungo Plaza.

Shughuli ya kufunga hotel hiyo imefanyika leo Novemba  9 asubuhi saa 12 huku wateja waliokuwa bado wamelala wakilazimika kuamshwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Scholastika Kevela amesema hotel hiyo inadaiwa kodi ya pango na Ubungo Plaza Sh.5.7 bilioni.

"Tunafunga na kukabidhi kwa mmiliki na shughuli hapa hazitaendelea tena hadi awe amelipa kodi," amesema Kevela

Mmoja wa wateja, Masoud Masoud akiwa na familia yake amesema''nimetoa hela nyingi na ilikuwa nikae kama wiki mbili na nimeingia jana, huu ni usumbufu."
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )