Thursday, December 21, 2017

Kanisa Katoliki kufanya misa ya Krismasi kitaifa Zanzibar

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limesema misa ya Krismasi kitaifa itaadhimishwa katika Jimbo Katoliki Zanzibar katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Minara Miwili.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Desemba 21,2017 na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano Jamii ya baraza hilo, Bernard James imesema misa hiyo itaongozwa na Askofu wa jimbo hilo, Mhashamu Augustino Shao.

Katika sikukuu hiyo inayoadhimishwa Desemba 25 ya kila mwaka, Wakristo duniani huadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

Awali, mratibu wa matukio ya kanisa Tumaini Media, John Leveti amesema Kardinali Polycarp Pengo ataongoza misa ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Maurus, Kurasini jijini Dar es Salaam.

"Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa yeye siku hiyo ya mkesha, Desemba 24 ataongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu Joseph," alisema Leveti.

"Siku ya sikukuu Kardinali Pengo atafanya ibada katika Kanisa la Mtakatifu Joseph na Nzigilwa atakuwa St Peters," amesema.

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )