Loading...

Monday, December 25, 2017

Klabu ya Galatasaray Yamuonea Huruma Eboue na Kumpa Dili Hili

Baada ya nyota wa zamani wa Ivory Coast Emmanuel Eboue kupoteza fedha zake kwa mke wake wa zamani hatimaye klabu ya Galatasaray ya Uturuki imempa nafasi ya kuwa kocha.

Eboue ambaye amewahi kutamba na klabu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Arsenal amepewa nafasi ya kuwa kocha msaidizi wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 14 (U-14) ya klabu ya Galatasaray.

Galatasaray imemtaka Eboue kushughulikia leseni yake ya kufundisha soka ili aweze kuanza kibarua rasmi ndani ya timu hiyo ili kuokoa hali yake ya kimaisha.

Klabu hiyo inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu soka ya Uturuki, imemwahidi mshahara mnono ili kusaidia kurejesha hali yake nzuri ya kimaisha.

Eboue amejikuta kwenye wakati mgumu wa maisha baada ya mahakama kuamuru mali zote kukabidhi kwa mke wake. Eboue na mke wake waliachana huku akiwa ameandika jina la mkewe katika sehemu kubwa ya mali zake ikiwemo nyumba za kifahari alizokuwa amezinunua kutokana na malipo yake kama mchezaji.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )