Loading...

Saturday, December 23, 2017

Mwalimu akamatwa kwa kubaka wanafunzi 9 wa darasa la kwanza

Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya mkoani Mara limemkamata na kumfikisha mahakamani Mwalimu wa Shule ya Msingi Itiryo kwa tuhuma za kuwabaka wanafunzi 9 wa darasa la kwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe, alithibitisha kuwa wamemkamata Mwalimu Swamwel Daniel ambaye anatuhumiwa kuwabaka wanafunzi wa darasa la kwanza wenye umri kati ya miaka 7 hadi 9.

Kamanda Mwaibambe alisema kuwa mwalimu huyo anadaiwa kutenda kitendo hicho kwa nyakati tofauti kati ya tarehe 30 Novemba hadi tarehe 6 Disemba. Aidha amesema walimkamata mtuhumiwa huyo alipokuwa akijiandaa kutoka nje ya nchi.

Mwalimu hiyo alifikishwa mahakamani Disemba 12 mwaka huu na kufunguliwa kesi ya jinai namba 682 ambayo inatarajiwa kutajwa Disemba 28 mwaka huu.

Aidha, Mwaibambe alisema kuwa ushahidi na vitu vyote vinavyotakiwa katika kesi hiyo vimekamilika na hivyo ameiomba mahakama kama itawezekana kesi hiyo isikilizwe ndani ya muda mfupi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )