Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, December 11, 2017

RC Gambo awavuruga CHADEMA...... Adai Mhe. Lema yupo mbioni kujiunga CCM

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewavuruga wanachama wa Chadema baada ya kuweka picha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akiwa na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na kuandika kuwa Lema yupo mbioni kurudi nyumbani.

Maneno aliyoambatanisha RC Gambo na picha aliyoiweka kwenye mtandao wa Instagram yalisomeka “Msituko yupo mbioni kurudi nyumbani!” jambo ambalo liliibua utata kwa baadhi ya wafuasi wa Chadema.
A post shared by Murriet (@mrisho_gambo) on
 
Tazama baadhi ya maoni ya wadau na wafuasi wa Chadema walivyopokea taarifa hiyo.
  • rexmyic—lema; mwenyewe sisi ccm hatumtaki mana hana sifa yakuwa huko@RC hide my ID
  • upendojlyahoo.co.uk—; Gambo acha we*u mchaga hadanganyiki wewe labda albat msando
  • jazzaluis_jr—; Acha kulisha watua maneno.kakuambia anarudi?amnaga kazi zakufanya
  • seif_71—; Badala ya kuongelea maendeleo kila siku kila mnawaza kuamisha wanachama kutoka kutoka huku kuingia huku mpk uchaguzi utafika ni hvy hvy tu!
  • momnathan2013–; Nunua wavulana wenzio sio Godbless Lema,mwanaume anaejitambua.
  • remmymosha—; Kuandika kwenyewe shida jembe letu haliwezi kwenda fisiem eti msituko badala ya mshtuko
  • neema7888; Old news …Tushawachoka sasa, WaTz tunataka maendeleo sio kuona watu wazima mkishindana kuhama vyama…old fools.!
Hata hivyo mpaka sasa Mhe. Lema hajaongea chochote kuhusu kauli hiyo ya RC Gambo. 

Je, kwa maoni yako unadhani Lema anaweza kuungana na CCM kama alivyofanya aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CUF, Maulid Mtulia. ?
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )