Loading...

Monday, December 18, 2017

Takukuru yatupa ushahidi wa Flashi ya Nassari, Lema

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema imeshindwa kuendelea na uchunguzi wa tuhuma za rushwa zilizowasilishwa na wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) na Godbless Lema (Arusha Mjini).

Msemaji wa TAKUKURU, Musa Misalaba alieleza sababu ya kufikia uamuzi huo kuwa ni wabunge hao kuharibu uchunguzi baada ya kuingiza siasa katika jambo hilo.

“Ni kweli flash tulikabidhiwa, lakini Nassari na mwenzake kwa sababu walivuruga uchunguzi hatuwezi kuendelea nalo. Unajua pale kilichofanyika ni kuendeleza kufanya siasa,” alisem Misalaba

Misalaba aliongeza kuwa wabunge hao waliligeuza jambo hilo kuwa la kisiasa na kufanya kuharibika kwa uchunguzi kwani hawakuwa wanawasilisha ushahidi wote kwa wakati.

“Ilionekana kama sanaa, hawakuwa na utayari wa kutuletea taarifa, walikuwa wanaleta kipande kidogo halafu kesho wanafanya kama mchezi wa Isidingo, kwa hiyo uchunguzi hauendi hivyo,” aliongeza Misalaba.

Takukuru imeeleza kuwa pamoja na kuwa na kiasi kidogo cha ushahidi, haiwezi kuendelea nao kwa sababu aliyepaswa kutoa ushahidi hakuwa tayari kushirikiana na taasisi hiyo huku akisema kuwa mmoja ya wabunge waliwasilisha ushahidi huo hakutokea pale alipotakiwa kuongeza taarifa zaidi za ushahidi.

“Ule haukuwa ushahidi, kuna mmojawapo tulimwambia aje kutoa ushahidi hakuonekana, matokeo yake wakawa wanaenda kwenye vyombo vya habari, kwa hiyo tunawaambia hatuwezi kufanya kazi kama hiyo. Sisi ni chombo huru kinachopaswa kufanya kazi bila kuingiliwa wala kushinikizwa na mtu,” alisisitiza .

Mbunge Joshua Nassari waliwasilisha ushahidi wa video ambao alidai kuwa unawaonyesha madiwani wa CHADEMA mkoani Arusha waliohamia CCM wakati wa ziara ya Rais Magufuli mkoani humo kuwa walinunuliwa kwa rushwa.

Madiwani hao walieleza kuwa wamejiuzulu nafasi zao na kujivua uanachama kisha kuhamia CCM kutokana na kuvutiwa na utendaji kazi pamoja na kumuunga mkono Rais Magufuli.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )