Monday, December 11, 2017

TANESCO Yawatoa Hofu Wateja Wake Juu Ya Mfumo Wa Ununuzi Wa Luku

Shirika la Umeme Tanzania Tanesco limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa ununuzi wa Umeme kwa njia ya luku na kusema kuwa kwa sasa upo sawa na wanaweza kununua
katika mifumo iliyozoeleka.

Akizungumza jana  jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano(TEHAMA) wa Tanesco, Demetruce Dashina alisema kuwa kulitokea tatizo dogo la mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya Luku kutokana na wataalamu wa shirika hilo walipokuwa wakihamisha mitambo hiyo kutoka ofisi ya Zamani kwenda sehemu nyingine.

“Jana tulikuwa tunafanya uhamisho wa mfumo wa luku kwenda katika ofisi zetu mpya hivyo ikawalazimu wateja wetu kupata usumbufu kidogo, lakini kuanzia saa saba(jana) mfumo huo umekaa sawa na wateja wanaweza kununua umeme kama walivyokuwa wanafanya hapo awali bila shida yoyote mara baada ya marekebisho ya kiufundi” alisema Dashina

Alisema kuwa shirika lilijipanga kuwahudumia wateja wake kama kawaida wakati wa kuhamisha mitambo hiyo lakini Wananchi wengi wakapata taharuki hivyo kufanya mfumo wa
ziada kuzidiwa kutokana na watu kununua umeme kuliko Kawaida.
 
Kwa upande wake Kaimu Meneja  Uhusiano wa Tanesco Leila Muhaji aliwaomba radhi wananchi kwa usumbufu uliojitokeza na kuwasisitiza kuwa sasa wanaweza kununua katika mifumo iliyozoeleka.

Muhaji alisema kuwa Tanesco inatambua umuhimu wa umeme hivyo   kuwataka watanzania kuwa na Imani na shirika lao kwani lipo kwa ajili ya kuwahudumia  kama inavyohitajika.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )