Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, December 23, 2017

Tanzania yasisitiza kuzidisha ushirikiano DRC

Waziri wa ulinzi wa Tanzania Hussein Mwinyi akipokea maelezo katika kambi ya MONUSCO Beni 

Waziri wa ulinzi wa Tanzania, Hussein Mwinyi ametoa wito wa kudumisha ushirikiano kati ya pande zote zinazo shiriki katika kuleta amani mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mwinyi alitoa wito huo siku ya Ijuma alipowatembelea wanajeshi wa Tanzania wanaoshiriki katika kikosi cha kimataifa cha kulinda amani mashariki ya Congo, na kuwatembelea wanajeshi waliojeruhiwa wakati wa shambulizi la Disemba 7, 2017.

Wanajeshi 14 wa Tanzania wa kikosi maalum cha nchi za Kusini mwa Afrika SADC waliuwawa na wengine 44 kujeruhiwa walipo shambuliwa na waasi wasiojulikana hadi hii leo katika kambi yao huko Semulik, karibu na mji wa Beni.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Beni, Waziri Mwinyi alisema amefika kuwapa pole wanajeshi wa Tanzania na kuwatembelea walojeruhiwa pamoja na kuwapa moyo kuendelea na jukumu lao la kurudisha amani katika eneo la mashariki ya Kongo.
Akizungumzia uchunguzi unaoendelea kuhusu shamblizi hilo, Mwinyi amesema hadi sasa hawana habari zaidi, "sasa hivi ni mapema sana kusema fulani amefanya hivi. Hatuna uhakika, UN pia haina uhakika na ndiyo maana tunasema ni lazima uchunguzi ufanyike."

Anasema uchunguzi ukifanyika utawawezesha kujipanga vyema zaidi ili tukio kama hili lisitendeke tena au likitendeka wawe tayari kukabiliana nalo, akitoa wito wa ushirikiano wa karibu zaidi kati ya pande zote zinazohusika na shughuli za kulinda na kurudisha amani mashariki ya Kongo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )