Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, January 13, 2018

Bunge bado halijamuita Ole Sendeka Kumuhoji

Bunge bado halijamuandikia barua ya kumuita Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka ili kujibu tuhuma za kukejeli na kudharau muhimili huo.

Katibu wa Bunge Stephen Kigaigai amesema kuwa bado hawajamuandikia barua ya kumwita kufika katika kamati hiyo.

"Niko katika kikao lakini ninachofahamu kuwa bado hatujamuandikia," amesema Kigaigai.

Januari 9 mwaka huu Spika wa Bunge, Job Ndugai aliagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumuita na kumhoji Sendeka wakati wa uchunguzi wa kamati hiyo kuhusu tuhuma hizo zilizonukuliwa katika mitandao ya jamii kwa lugha ya Kimasai, Kiswahili na Kingereza.

Spika alisema lengo la kumuita ni kubaini ukweli wa dhamira ua kauli hizo na lutoa mapendekezo kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa na Bunge.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )