Monday, January 15, 2018

Cyprian Musiba atangaza kumshitaki Tundu Lissu

Mkurugenzi Mkuu wa CZ Information & Media Consultant LTD, Cyprian Majura Nyamagambile leo January 15, 2018 amezungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa yeye na baadhi ya Wanasheria nchini katika siku mbili zijazo watamfungulia mashtaka Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

Ameeleza kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na maneno aliyoyatoa Lissu kabla ya kwenda nchini Ubelgiji kwaajili ya matibabu, kwa kutoa kauli nzito kuwa Tanzania kwasasa sio mahali salama pa kuishi na eneo hatarishi kwa maisha ya binadamu.

Musiba ameeleza kuwa kauli hizo zililenga kuidhalilisha nchi, kuwapa hofu wageni wanaokuja nchini kwa ajili ya kutalii lakini pia kuwaogopesha wananchi washindwe kufanya kazi zao kwa amani na hivyo wanahitaji aisaidie nchi kutoa uthibitisho wa kauli zake hizo katika vyombo vya sheria.

“Tunampa siku mbili atoe uthibitisho wa kauli zake vinginevyo tutampeleka mahakamani, na japokuwa tutampeleka katika mahakama za ndani, nakala yake itapelekwa The Hague Uholanzi kwenye Mahakama ya Kimataifa.” Amesema Cyprian Musiba

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )