Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 16, 2018

Dr Mashinji (Katibu Mkuu) Azungumzia Nafasi ya Uenyekiiti Ndani ya CHADEMA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vicent Mashinji amefunguka kuhusu nafasi ya uenyekiti ndani ya chama hicho.

Mwanasiasa huyo amesema mwanachana yeyote wa Chadema anaweza kuwa Mwenyekiti ila kwa sasa ni wakati wa Freeman Mbowe ambaye ndiye anashikilia nafasi hiyo.

“Chadema ni chama ambacho kina fursa na kila mtu na mwanachama yeyote anaweza kuwa Mwenyekiti lakini watu waelewe huu si wakati wake ni zamu ya Mhe. Freeman Mbowe ukifika wakati wa uchaguzi atakuja mtu mwingine,” amesema Dkt. Mashinji.

“Mfumo wetu ni tofauti na CCM, chama kinaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Rais amevaa kofia mbili kwa utawala bora hili haliwezekani sababu chama kinatakiwa kuongozwa na Mwenyekiti ambaye anatakiwa pia kuisimamia Serikali,” ameongeza.

Pia amesema toka miaka ya 90 Mhe. Mbowe alikuwa Mwenyekiti wa vijana lakini watu wanasahau kuwa bado hiki ni kipindi cha uongozi wake na bado haujamalizika.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )