Wednesday, January 24, 2018

Jaji mstaafu Robert Kisanga afariki dunia

Jaji Mstaafu Robert Kisanga amefariki dunia  katika Hospitali ya Regence ya Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Msajili wa Mahakama ya Rufaa, John Kahyoza.

Mbali na Mahakama ya Rufaa, Marehemu Jaji Robert Kisanga alifanya kazi Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Pia amewahi kuwa mwenyekiti wa kwanza wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini ambapo alistaafu mwaka 2008.


Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )