Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, January 10, 2018

Kauli ya Tundu Lissu Baada ya Lowassa Kwenda Kuonana na Rais Magufuli Ikulu

Baada ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kumtembelea Rais Magufuli Ikulu Leo January 9, 2018 Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu  ambaye yupo nchini Ubelgiji kwa ajili ya matibabu ametoa mtazamo wake kuhusu suala hilo

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Lissu amepost picha inayomuonesha Lowassa akiwa Ikulu na kuandika maelezo haya; “Na hatukatai kuzungumza na Magufuli kuhusu matatizo mengi na makubwa yanayoikabili nchi yetu.”

“Lakini ni muhimu na lazima viongozi wakuu wa chama washirikishane na washauriane kabla ya mazungumzo hayo. Na baada ya mazungumzo, ni lazima viongozi wakubaliane juu ya kauli za kutoa hadharani kwa umma ili wote tuwe kwenye ukurasa mmoja.

“Viongozi na wanachama wetu wanashambuliwa hadharani kwa mapanga na hata kwa risasi, kumsifia Rais ni kumuunga mkono yeye. Katika mazingira ya kesi nyingi za kutunga dhidi yetu, ‘kazi nzuri’ inayofanywa ina maana gani, kama sio kuhalalisha ukandamizaji tunaofanyiwa.

“Katika mazingira ambapo hata jumuiya ya kimataifa imeanza kuhoji mwenendo wa Rais Magufuli, kutoa kauli kwamba ‘anafanya kazi nzuri’ ni ‘kumtupia taulo’ la propaganda litakalomfichia madhambi mengi aliyowafanyia Watanzania katika miaka hii miwili.

“Kwa vyovyote vile, kitendo cha Lowassa sio cha kunyamaziwa au kuhalalishwa kwa hoja nyepesi nyepesi.”– Lissu
2: Na hatukatai kuzungumza na Magufuli kuhusu matatizo mengi na makubwa yanayoikabili nchi yetu. . Lakini ni muhimu na lazima viongozi wakuu wa chama washirikishane na washauriane kabla ya mazungumzo hayo. . Na baada ya mazungumzo, ni lazima viongozi wakubaliane juu ya kauli za kutoa hadharani kwa umma ili wote tuwe kwenye ukurasa mmoja. . Katika mazingira ya sasa, ambako viongozi na wanachama wetu wanashambuliwa hadharani kwa mapanga na hata kwa risasi, kumsifia Rais ni kumuunga mkono yeye na matendo yake. . Katika mazingira ya kesi nyingi za kutunga dhidi yetu, 'kazi nzuri' inayofanywa na Magufuli ina maana gani hasa, kama sio kuhalalisha ukandamizaji tunaofanyiwa. . Katika mazingira ambapo hata jumuiya ya kimataifa imeanza kuhoji mwenendo wa Rais Magufuli, kutoa kauli kwamba 'anafanya kazi nzuri' ni 'kumtupia taulo' la propaganda litakalomfichia madhambi mengi aliyowafanyia Watanzania katika miaka hii miwili. . Kwa vyovyote vile, kitendo cha Mheshimiwa Lowassa sio cha kunyamaziwa au kuhalalishwa kwa hoja nyepesi nyepesi.
A post shared by TUNDU ANTIPHAS LISSU (@tundulissutz) on
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )