Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, January 17, 2018

Keshi Ya Agness Masogange Yakwama Tena Mahakamaniu

Upande wa mashtaka katika kesi ya  kutumia dawa za kulevya inayomkabili Agnes Gerald maarufu kama ‘Masogange’ umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwaonya  upande wa utetezi kwa kushindwa kutoa ushahidi  wao  kwa mara ya tatu mfululizo.

Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa wakili mwenzake, Reuben Simwanza ndiye aliyeandaa mashahidi na kwamba ameshindwa kutokea kwa kuwa anaumwa.

Wakili wa Serikali, Constantine Kakula alitaka upande huo uonywe leo Jumatano baada ya shauri hilo kufikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Kutokana na hali hiyo, Wakili Nkoko amesema atahakikisha anaandaa mashahidi ili itakapotokea wakili mmoja hayupo, mwengine aendelee na shauri.

"Hatuna pingamizi na sababu zilizotolewa na upande wa utetezi lakini tunaomba  Mahakama itambue kuwa ni mara ya tatu kwa upande wa utetezi inaahirishwa kesi hii? Amesema wakili wa Kakula na kuongeza;

"Mawakili wapo wengi lakini wanashindwa kuendelea kutoa ushahidi wao wa upande wa utetezi basi kama hawawezi, waache mshitakiwa aendelee na kesi mwenyewe."

Kutokana na hali hiyo, upande wa mashtaka umeomba ahirisho la mwisho kwa sababu kesi ni ya muda mrefu.

Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 26, mwaka huu  kwa ajili ya kusikilizwa.

Masogange ataanza kujitetea baada ya Mahakama kumkuta na kesi ya kujibu baada ya kusikiliza mashahidi watatu wa upande wa mashitaka.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )