Loading...

Monday, January 29, 2018

Necta yatangaza tarehe ya mtihani kidato cha sita

Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limesema mitihani ya kuhitimu kidato cha sita itaanza Mei 7 hadi 24, 2018.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Necta Januari 26, 2018 inaonyesha somo la kwanza litakuwa ni masomo ya jumla ‘General Studies’ na somo la mwisho litakalofanyika Mei 24 litakuwa ni Baiolojia 3C (kwa vitendo).

Msemaji wa Necta, John Nchimbi amesema “lengo la kutoa ratiba ni kuwafanya wanafunzi na walimu wao kujiandaa kwa ajili ya mitihani yao.”

“Ratiba inawasaidia wao kuweza kufanya maandalizi lakini kuwaweka sawa kisaikolojia  na kujua mitihani ipo, itakuwa lini hadi lini na muda gani,” ameongeza
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )