Thursday, January 4, 2018

Polepole atishia kung’oa kigogo Mwingine wa CHADEMA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ametishia kung’oa kiongozi mkubwa wa Chadema ndani ya mkoa wa Dar es salaam.

Ameyasema hayo mara baada ya madiwani wawili wa CHADEMA  kuachia ngazi Mjini Iringa, ambapo amesema kuwa hoja za madiwani hao wanakimbia ubabe wa mchungaji Msigwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo.

"Leo Madiwani wengine wawili wamehama na kujiunga na CCM. Ukiwasikiliza kilichowaondoa ni Uongozi Mbovu na Ubabe pale Iringa Mjini. Nasikia wameambiwa "never outshine your master". Mimi nilidhani "masta" ni wananchi kumbe ni "pasta". Ukitukana tusi moja Kiongozi mmoja nachomoa DSM " Ameandika  Polepole

Siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la viongozi wa kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) kuhamia chama tawala cha CCM.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )