Loading...

Tuesday, January 16, 2018

Polisi Dar Watoa taarifa juu ya oparesheni iliyofanywa na Jeshi la Polisi katika kuwakamata wahalifu

Jeshi la Polisi kanda Maalumya Dar es Salaam limekamata silaha mbalimbali zikiwemo bunduki, bastola na vifaa vingine vya kufanyia matukio ya uhalifu pamoja na watuhumiwa mbalimbali wa makosa ya uhalifu ambao walikuwa wakijiandaa kutekeleleza matukio hayo.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasaamesema jeshi hilo limekamata silaha aina ya AK 47 na watuhumiwa wawili nyumbani kwa mzee Said Omary (62) baada ya kupata taarifa kuwa kuna wahalifu wanataka kufanya tukio la wizi wa kutumia silaha.

Aidha Polisi imewakamata watuhumiwa 2 wa wizi wa magari ambao baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na radio call, kadi 10 za benki mbalimbali, leseni za udereva, master keys 15 ambapo baada ya kuhojiwa walikiri kutekeleza matukio mbalimbali ua uhalifu huku wakionesha magari mawili na pikipiki moja vinavyodhaniwa kuwa ni vya wizi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )